Loading...

BREAKING NEWS: WATU 26 WAMEFARIKI KATIKA MASHAMBULIO MAKALI YALIYOZUKA MUDA HUU

MoshiImage copyrightRozina Sini News
Image captionMoshi umeonekana ukitoka kwenye moja ya majumba katika uwanja huo
Watu 26 wamefariki baada ya mashambulio kutekelezwa katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek mjini Brussels.
Waziri wa afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki na wengine 81 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya mji wa Brussels.
Kampuni inayosimamia uchukuzi wa treni Brussels imesema kwamba watu 15 walifariki Maelbeek na wengine 55 kujeruhiwa, 10 kati yao wakijeruhiwa vibaya.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mashambulio hayo mjini Brussels na kusema ni kama mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top