Loading...

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Rais Dk John Magufuli kuacha ‘kutumbua majipu’ bila kufuata taratibu na kanuni za nchini.




Dk. Vicent Mashinji

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Rais Dk John Magufuli kuacha ‘kutumbua majipu’ bila kufuata taratibu na kanuni za nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji, wakati alipokuwa akifungua kongamano la Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) na Umoja wa wanachadema Vyuo vikuu (Chaso) mjini hapa.
Dk. Mashinji alisema kuwa tangu aingie madarakani Rais Magufuli amekuwa na utalatibu ambao umepewa jina la utumbuaji majipu ambao amekuwa akiuendesha bila kufuata sheria za nchi.
Alisema kuwa pamoja na kuwa Chadema wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawakotayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi.
“Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,”alisema Dk, Mashinji.
“Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.
Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake.
“Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,”alisema.
Aliwataka vijana wa vyuo vikuu nchini kuungana na Chadema katika kuhakikisha serikali inaruhusu kuonyeshwa kwa vipindi vya Bunge moja kwa mpja kama ilivyo kuwa hapo awali.
“Bunge maana yake ni mkutano wa hadhara ambao wote tunatakiwa kushiriki lakini kutokana na udogo wa eneo wanakwenda wawakilishi wetu lakini na sisi tunatakiwa tufuatilie kupitia runinga zetu moja kwa moja ili tuweze kujua kinachofanywa bungeni na wawakilishi wetu,”alisema.
Pia aliwataka vijana kuacha ushabiki wa kushabikia siasa bali waikosoe serikali ili iweze kufanya kazi ambayo ni kuwaletea maendeleo wananchi wake kwakua huo ndio wajibu wake.
Akizungumza na wenyeviti wa CCM wa Mikoa na Wilaya Ikulu, Rais Magufuli alisema wanaotetea watu wanaotumbuliwa na wao ni majipu hivyo ataanza kuwachunguza.
Alisema inasikitisha kuona watu wanatetea watumishi ambao wamekuwa wakiwaibia watanzania miaka mingi lakini wanapofukuzwa kazi wanalalamika.
“Kama wamekuwa wakiwaibia wananchi hadharani nasisi tutawafukuza na kuwatangaza hadharani, inasikitisha kuona baadhi yetu tunatetea watu wanaofukuzwa kazi,” alisema Rais Magufuli

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top