Loading...

Obama na Castro wajibizana Cuba

ObamaImage copyrightReuters
Image captionBw Obama na Bw Castro wamejibizana kuhusu haki za kibinadamu
Rais Barack Obama na mwenyeji wake Raul Castro wamejibizana kuhusu suala la haki za binadamu na vikwazo vya kibiashara baina ya Marekani na Cuba.
Hata hivyo Rais Obama amehimiza Cuba kuendelea na mageuzi ya kisiasa na haki za binadamu kama inataka kurejesha ambao kwa miaka mingi ulidorora baina ya mataifa hayo mawili.
Lakini Castro naye ameishutumu Marekani na kusema ina unafiki.
Ameitaka iondoe vikwazo vya kibiashara ilivyowekea Cuba na pia kuitaka irejeshe eneo la Guantanamo. Marekani imejenga gereza la kuwazuilia washukiwa wa ugaidi katika eneo la Guantanamo Bay.
Katika siku ya pili ya ziara yake ya Kihisitoria nchini Cuba, rais Obama amesema kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo la Kikomonisti kutategemeana na uharaka wa mataifa hayo mawili kuondoa tofauti zao hasa katika suala la haki za binadamu.
CubaImage copyrightAFP
Image captionMarekani imekuwa ikifufua uhusiano wake wa kidiplomasia na Cuba chini ya Obama
Obama amesema kuwa Marekani haioni kama Cuba ni tishio kwa Marekani na kwamba ziara yake nchini humo ina lengo la kuweka misingi mipya kati ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Rais Obama baada ya mazungumzo ya mjini Havana na mwenyeji wake Raul Castro, amesema kutokuwepo harakati za kupigania haki za binadamu nchini Cuba ni jambo litakalo mpatia ugumu kushawishi bunge la Congress kuondoa vikwazo vilivyopo dhidi ya Cuba.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top