Loading...

BREAKING NEWS: SERIKALI YA MAGUFULI YAFANYA KUFURU KWA UKAWA IMEAMUA KUTOA MAJIBU MAKALI NA KUWAKATA MAINI KWA HOJA ZAO


SIKU moja baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kususa kuchangia hotuba za bajeti, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri,
amesema serikali haikukosea kuipa Wizara ya Ujenzi fedha zaidi ya zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge.
Hoja hiyo ni moja kati ya tatu ambazo juzi ziliibuliwa bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Badala ya kuwasilisha Mpango Mbadala wa Maendeleo wa Taifa na maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mpango wa serikali pamoja na maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu, juzi Mbowe alisema wabunge wa upinzani watakuwa wanaingia kwenye Ukumbi wa Bunge lakini hawatachangia hotuba ya bajeti mpaka pale hoja zao zitakapojibiwa.
Mbowe alidai kuwa uamuzi wao huo umetokana na Serikali kufanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji kazi kwa wizara mbalimbali, kuvunjwa kwa Katiba na sheria za nchi na kupokwa uhuru na madaraka ya muhimili wa Bunge.
Mwenyekiti huyo wa Chadema na Mbunge wa Hai, alikwenda mbali zaidi akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekiuka sheria kwa kuipatia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sh. bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2015/16 wakati Bunge liliidhinisha Sh. bilioni 191.6.
Wakati Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyeongoza kikao cha juzi akieleza kuwa madai ya upinzani ni mazito na kushauri waende mahakamani, Serikali imejibu moja ya hoja tatu za Mbowe.
MMAJIBU KWA MBOWE
Katika mahojiano maalum na Nipashe kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango mjini hapa jana asubuhi, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Mwanri, alisema Serikali ya Awamu ya Tano haijafanya makosa kuipa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kiasi hicho cha fedha.
Ofisa huyo wa serikali alisema Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 inaruhusu Ofisa Masuhuli na Waziri kufanya uhamisho wa fedha za mradi mmoja kwenda kutekeleza mradi mwingine.
"Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 inaruhusu Ofisa Masuhuli kufanya 'reallocation' (uhamisho) ya matumizi ya fedha lakini isizidi asilimia saba ya 'Vote' (Fungu) husika,

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top