Loading...

Bundi wa ugoni atua kwa Askofu Malasusa

DK. Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani
Dk. Malasusa anadaiwa kuwa na uhusiano na Leita Ngowi, mchungaji na mkurugenzi wa idara ya wanawake usharika wa Azania Front, Jijini Dar  es Salaam aliyepandishwa cheo siku za karibuni na askofu huyo.
Akizungumza na MwanaHALISI kwa simu leo baada ya kunusurika na mateso ya polisi waliodaiwa kumweka rumande kwa maelekeo ya viongozi wa jeshi hilo wenye uhusiano na Dk Malasusa, Mwakilima amesema “Askofu ananichukulia mke wangu.”
Ameahidi kusema zaidi wiki hii.
Anasema mkewe ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambaye walianza uhusiano kama marafiki, baadaye wakaamua kuwa mke na mume. Mwakilima anasema alifanikiwa kumsomesha mkewe katika Chuo Kikuu cha Makumira hadi akawa mchungaji.
Anadai kuwa tangu 21 Machi mwaka huu, uhusiano wake na mkewe umevurugika kwa sababu ya mzozo uliotokana na kile anachoita “uhusiano wa kimapenzi na Askofu.”
Anasema alishtuka baada ya kufuma wawili hao wanatumiana ujumbe wa simu wa kukutana kufanya mapenzi maeneo mbalimbali.
Baada ya mume kuanza kufuatilia, mke wake alipandishwa cheo haraka na kuwa mkurugenzi wa wanawake katika Usharika wa Azania Front yalipo makao makuu ya dayosisi hiyo.  Akapeleleza na kukuta kuna udanganyifu anaofanyiwa katika ndoa yao, kukazuka ugomvi kati yake na mkewe.
Baada ya kubaini kwamba mkewe alikuwa ameumia katika ugomvi huo, akampeleka Hospitali ya TMJ kwa matibabu. Kwa sababu ya haraka, alisahau kadi ya bima yake. Akalazimika kumwacha pale mkewe na kurudi nyumbani kuchukua kuichukua kadi hiyo.
Mwakilima amesema kuwa aliporejea alikuta mkewe ameondolewa na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akaambiwa na wauguzi kuwa aliyemhamisha mkewe ni Askofu Malasusa.
Alipokwenda Muhimbili alikuta askari wanalinda wodi, wakamzuia kuingia wodini kwa maelekezo ya Dk. Malasusa. Akiwa bado anabishana na polisi, Malasusa alijitokeza akiwa aamebeba chakula kwa ajili ya  mgonjwa wake huyo.
“Tafrani ilizuka, nikahoji iweje mke wangu  anahudumiwa na Askofu wakati mimi nazuiwa kumwona. Pale pale, Askofu alipompigia Paul Makonda, akatuma askari nikachukuliwa kuswekwa ndani kituo cha polisi Wazo -Tegeta,” anasimulia.
Nikiwa Tegeta mmoja wa askari aliniambia, “hii kesi ina amri nyingi, ina watu wengi wanaoisakama, inaweza kukuingiza matatizoni.”
Hivyo askari wa Wazo  waliamua kujinasua na sakata  hilo na kunipelekea Kibaha, ambapo sasa nimeambiwa nitafikishwa mahakamani kwa kosa la kujeruhi.
Mume huyo amesema aliporejea nyumbani kwake alikuta hata watoto watatu aliozaa na mkewe wametoroshwa kwa maelekezo ya Askofu Malasusa, na alipofika kituo cha polisi wazo hakukubaliwa kufungua shitaka dhidi ya kiongozi huyo wa dini.
MwanaHALISI limemuuliza Askofu kuhusu sakata hili, alidai yupo kikaoni. Alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu pia.
Mchungaji huyo wa kike anayetuhumiwa  kuwa na uhusiano mbaya na Askofu, amekiri kuwa mumewe amekuwa anamhusisha na kuhusishwa na kiongozi huyo wa iroho, lakini alisisitiza kuwa amachotaka ni mumewe kumkamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa madai kuwa anamnyanyasa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top