Loading...

Mange Kimambi Afunguka Kuhusu Video ya Msichana Aliyepigwa Video Akiwa Uchi na Kubakwa Morogoro

Blogger maarufu Mange Kimambi ameguswa na tukio la msichana kurekodiwa video akiwa uchi na kulazimishwa kufanya mapenzi na kisha video kusambazwa mitandaoni , ameandika haya katika ukurasa wake wa Instagram

mangekimambi_ Jamani watz tuachage kutengeneza story za uwongo. Ile story ya facebook yani walaaa. So issue iko hivi, Huyu dada alikuwa anatoka na bosi wa matrekta huko vijijini- Morogoro. Dizain jamaa kaoa ana familia yake so demu na yeye akawa anachepuka na mtu mwingine wa saizi yake. Ndo huyo jamaa kuambiwa kuwa demu anam cheat ndo akamuita hapo lodge, inaitwa Tiff Lodge iko Dakawa-Morogoro(jina la lodge limeandikwa kwenye mashuka, nimeona kwenye video)Demu akaenda akijua anaenda kuonana na jamaa yake hakuna issue, Kumbe jamaa keshampanga huyo njemba aje kumbaka alafu yeye akae arekodi then asambaze kwenye social media.Imagine Huyu jamaa alivyomind demu kuchepuka mpaka kumdhalilisha dada wa watu hivi utasema alikuwa na plan za kumuoa au hata kumchumbia kumbe ni mume wa mtu.
.
Huyu binti kwanza anamuogopa huyo jamaa kufa. Baada ya kufanyiwa huu unyama alipofika nyumbani alimweleza mamake Ila binti aligoma kabisaaa kwenda polisi, mama yake ndo akaenda polisi, polisi nao wakagoma kufungua kesi mpaka binti aende mwenyewe. Yani unaambiwa hiyo kumfanya binti akafungue kesi tu ilikuwa mshike mshike, nasikia ni baada ya hii video kusambaa ndo akakubali kufungua kesi. Jamani Huyu binti Inabidi mtu amshikee ampe moyo mpaka siku atakayoingia mahakamani kutoa ushahidi la sivyo hachelewi kuogopa... Lakini uzuri wa hii kesi serikali wala haimuhitaji sana mlalamikaji yani video inajielezea yenyewe.
.
Sasa jamani naomba tushirikiane hapa. Hawa jamaa wako ndani kesho ndo wanafikishwa mahakamani . Mkuu wa wilaya ya Mvomero- Morogoro ambako ndo issue ilipotokea ni Betty Mkwasa na yeye keshapewa habari hii, Ila Sasa it seems polisi hawana hizi video. .Nimepewa number ya Betty Mkwasa Ila nashindwa kumuadd whatsapp Naomba mtu amwambia ani add nimpe hizo video +1 424 333 2650, Au Nyie wadau ambao mnazo hizo video na mnaijua number ya Betty Mkwasa pls mtumieni ili azifikishe polisi leo hiii Kabla ya Kesho mahakamani. Jamani hawa mbwa wasipate dhamana Kesho... Also nyinyi ambao mnazo hizi video Tafadhali msimtumie mtu yoyote yule Maana tunazidi kumdhalilisha huyo dada kwa kuzisambaza.Kama unataka kumsaidia huyo dada zikifishe video polisi ya Mvomero - Morogoro leo hiii....

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top