Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaanza kuwatumbua viongozi wa ngazi za chini ambao wataisababishia Serikali upotevu wa mapato wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika bajeti ya Mwaka 2016 /17.
Kauli hiyo ameitoa mjini Dodoma katika ufunguzi wa semina ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma ambapo Mama Samia amesema kuwa utumbuaji wa majipu hautakuwa kwa viongozi wa ngazi ya juu tu bali pia utakuwepo kwa viongozi wa ngazi za chini.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewataka viongozi hao kwenda kuisimamia serikali kutekeleza majukumu yake.
Kwa upande wake ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Kongwa,ametaka kutungwa kwa Sheria ndogo ambayo itawapa haki Sadiwani ya kuwawajibisha viongozi wanaotafuna mali za Umma.
Post a Comment