Kama unavojua wabongo Umbea una nguvu kuliko Ripoti ya CAG insta kumechafuka.....Mama Diamond alianza kwa kufuta picha zote alizo post za Zari watu wakasema Mmmmmmmmh kuna kitu hapa,(mimi sidhani kama kufuta picha za mtu ni kitu kibaya lakini hakufuta za zari tuu mbona hata za wengine alifuta akaacha za Tiffa na Rommy tuu)
Wafuatiliaji wa mambo hawakuishia hapo wakasema Esma dada wa Diamond Ka muunfollow Zari (sina uhakika lakini Kwa usawahili wa huyu Dada nilishangaa kuona anapatana na Zari huyu ni mswahili mno na Diamond asipo kuwa Makini atamponza kwa uswahili wake)
Watu wakaendelea na story kwanini Zari hakutoa shout out kwa wimbo wa Raymond video ya Kwetu wakaguna wakasemaaa mmmmmmmmh hapa kuna kitu huenda Diamond anatoka na yule video queen wa hio video(Sioni tatizo tukumbuke Video ilitoka wakiwa bsy ulaya hata Mama Dai naye hajatoa Shout out kwenye video na hata picha alio post kuhusu hio video hamna)
Wafuatiliaji wa Mambo wakasema ishu ilianza kutokea world tour kuwa wakati wa kurudi kila mtu alipita njia yake Mama Diamond na Zari (mimi sioni Tatizo as long as Zari anaishi South Africa huenda alichukua ndege moja kwa moja hadi South na Mama Dai akaja bongo)
Juzi juzi hapa Dai na Zari wamepost picha zao wakionesha they are happy na mahusiano yao so Sidhani kama kuna kitu hicho ingawa leo bado hawajapost chochote
Kimbembe ni pale Mama Dai alipo like picha ya Video queen(anaesadikika kutoka na Dai)
Watu wakaendelea kupagawa na kuona kama yasemwayo yanaukweli baada ya video queen kupost picha hizi (Lakini ameshazifuta ila wajanja waliwahi)
MTAZAMO:
Kama Dai atakuwa kweli kaamua kuachana na Zari (Sidhani kama kitatokea) na kuja Kutoka na Video queen kwanza atakuwa amejishushia heshima yake hata kama Mama Dai ndo anampenda huyo video queen!, pili Dai atakufa Maskini maana wabongo huyo video queen atahamishia hadi ukoo wake pale white house sasa itakuwa bila bila Dai yupo na kijiji chake na huyu yupo na Kijiji chake!
Kingine ni kuwa Dai akae na dada zake na Mama ake awambie wapunguze uswahili kwa Zari! Utakuja kumponza Esma ni mswahili sana bora hata Halima! Esma yake yanamshinda anataka kuvuruga ya watu,pia Mama ake hata kama Insta kaikutia ukubwani Apunguze uswahili mwanae ashakuwa super star,yeye atulie afaidi matunda basi uswahili wakumuamlia atoke na nani ni ujinga na atampotezea mwanae Heshima!
Pamoja na kuwa zari ni mvumilivu namshauri Dai apunguze watu wakukaa nae Nyumbani kwake ana nyumba nyingi sio kila mtu lazima akae nae hata kama huruma sasa zinazidi! Ile ni nyumba yake na mke wake ndo maana ya mke,mama mkwe awe na nyumba yake,dada zake pia na ndugu wengine zari atakuwa anakosa uhuru ajifunze mbna Zari haleti ndugu zake! Ndoa ni kitu nyeti sana!
Napinga kwa asilimia 80% kuwa Dai anatka kumtosa Zari kwenda kwa video queen mtoto! Lakini ngoja tuone hii ngoma itaishia wapi
Reality Tv show ya Daimond huenda ikawa inatafutiwa Kiki kwa njia hii,mama Dai wabongo asha wajua kuwa akitoa Show yake hyo itauza maana wengi wanapenda umbea so huenda ni kiki
Mchezo huu hauhitaji hasira
Post a Comment