Loading...

LISSU ATAJA MADHARA YA KAULI YA HAPA KAZI TU KWA JAMII

tundu lissu

tundu lissu

KAULI mbiu ya serikali ya Rais Dk. John Magufuli ya Hapa Kazi Tu imedaiwa kuwa imeongeza vitendo vya kikandamizaji kila mahali nchini.

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Waziri Kivuli wa Wizara ya Katiba na Sheria amesema kauli mbiu hiyo imeleta ukandamizaji katika baadhi ya maeneo hata kule ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kilikataliwa.

Alitolea mfano wa vitendo hivyo vilijitokeza katika Jiji la Tanga ambako CCM ilikataliwa na wananchi lakini ilitumia ghilba na mabavu ya kila aina kuhakikisha inanyakuwa Umeya wa jiji hilo.

Kutokana na ukandamizaji huo wa CCM, viongozi mbalimbali na madiwani waliochaguliwa na wananchi wanakabiliwa na mashtaka ya kutengenezwa kwa sababu tu ya kukataa kwao kutawaliwa na watu ambao hawakupata ridhaa ya wananchi.

Amefananisha kitendo hicho na kile na kilichotokea Halmashauri ya Kilombero ambako mbunge halali wa jimbo hilo alitolewa kwa nguvu na polisi ili CCM iliyokataliwa na wananchi kwenye kura iweze kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema katika Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri zake licha ya serikali kuwa na nguvu nyingi lakini wananchi na viongozi wao walifanikiwa kutetea maamuzi ya wapiga kura na kuzuia ubakaji wa kidemokrasia kwa kuweka mameya wa chama kilichotawala kwa nguvu ya wananchi kwenye uchaguzi.

“Haijalishi kwamba mawaziri hawa si mamlaka yao ya kinidhamu kwa utumishi wa umma na kama tulivyo onyesha wala hawajakamilisha majukumu yoyote ya kisheria sasa mawaziri wanafukuza au kusimamisha au kuwahamisha watumishi walio chini yao wakiulizwa hujibu hapa kazi tu” amesema Lissu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top