Loading...

TAMU YA TENDO LA NDOA

Couple lying in bed together

Linajenga ukaribu zaidi kwa wanandoa
Kutokana na majukumu ya kifamilia ambayo yanakua kwa kasi na kufanya baadhi ya wanandoa kutokuwa na ukaribu zaidi na wenzi wao.

Wanandoa wengine wamefaulu kwa kuhakikisha kuwa maran kwa mara wanawasiliana na wapenzi wao kujuzana haya na yale kuhusu mahusiano yao.

Kumwelewa mwenzi wako
Tendo la ndoa lina lugha yake na haliishi tu katika kufurahia na kufika kileleni bali pia linasaidia kumwelewa na kumsoma mwenzi wako. Ndio maana ni vyema kufahamu tabia ya mwenza wako na mwenendo kwa kuhusisha tendo hilo. Ikiwa wenza wana tabia ya kushirikiana na kuhusishana katika masuala ya kila siku ni rahisi kutambua kuwa mwenza wako siku hiyo kachoka, kachukizwa (iwe wewe ama na mtu mwingine), ana mawazo, ana wasiwasi au hana raha.

Inasaidia wanandoa kupata Watoto
Watoto wana raha yake katika ndoa, na wana nafasi kubwa  katika kuweza kuimarisha ndoa, kuleta furaha katika familia, huwajenga na huwakomaza wazazi na pia huwaunganisha zaidi wanandoa kama mwili mmoja. Si wote wamejaaliwa kupata watoto ila ukweli ni kwamba mara nyingi hiki ni kipengele muhimu katika ndoa ambacho wanandoa wenyewe na jamii hutarajia kufanikisha zoezi hili ili ndoa ionekane kuwa na mafanikio.

Kutatua migogoro baina ya wenza
Ugomvi haukwepeki hata kama wenza wanapendana hivyo tendo la ndoa linazungumza mambo mengi kwani kitendo cha kukutana kimwili na mwenza wako kinaifanya akili na mwili kukubali kuwa umejitoa kwa mwenzi wako kwa wakati huo.

Kupunguza uchovu na msongo wa mawazo

Ndoa ni moja ya njia inayotumiwa na baadhi ya wenza kuweza kupunguza msongo wa mawazo, tendo likifanywa vyema na kwa ustadi, huweza kumwondolea mwenzi wako  msongo wa mawazo kwa kiwango kikubwa.

Unafuu huo utegemea lakini, wengine inakuwa tu unafuu wakati wa tendo hilo na hali wengine hupata nafuu ya muda mrefu. Hivyo ikiwa mwenzi wako yupo katika hali hiyo katika kutafuta namna ya kuhakikisha anapata unafuu, unaweza tumia tendo la ndoa kama silaha ya kumrudisha mwenzi wako katika hali nzuri.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top