Loading...
Home
»
NEWS
»
HABARI YA HIVI PUNDE: CHADEMA SASA HAPAKALIKI WAZUA TAHARUKI KUBWA NA MGANGANO WA VIONGOZI NI BAADA YA KUTOA TAMKO HILI JUU YA SERIKALI HUKU MWALIMU AKIFUNGUKA KWA UCHUNGU ZIDI SAKATA HILI KWELI CHADEMA SASA WALIPOFIKIA NI BALAA....
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza rasmi kutoitambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inayoongozwa na Dk Ali Mohamed Shein.
Mbali na kutoitambua Serikali hiyo, chama hicho kimesema leo kitatoa mkakati mzito wa namna ya kushughulikia suala la matangazo ya Bunge la Kumi na Moja kutoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni.
Msimamo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari jana mjini Dodoma katika kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, manaibu wake wawili, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Pia walitoa taarifa juu ya mambo yanayojadiliwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu (CC) kinachofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, Mwalimu alisema chama hicho hakitampa ushirikiano Dk Shein.
“Kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi Jumatatu, tumefikia msimamo wa kutoitambua Serikali ya SMZ. Msimamo wa Maalim Seif Shariff Hamad ndiyo msimamo wetu,” alisema.
Maalim Seif aliwania urais Zanzibar kupitia CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kabla ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta matokeo yake na kutangaza uchaguzi wa marudio ambao mgombea huyo na chama chake walisusia.
“Hatutatoa ushirikiano kwa SMZ na katika kikao cha leo (jana) cha CC tutawasilisha azimio hilo.Hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya mbaya sana. Wazanzibari wanaelekea kununa,” alisema Mwalimu.
Mwalimu alisema hawatafanya maandamano Zanzibar lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwani Wazanzibari wengi wanaelekea kununa na kwamba hilo litasababisha hali mbaya zaidi.
“Hali ya Zanzibar si nzuri kama CCM wanavyoeleza. Watu hawazikani, hawatembeleani tumerudi kulekule kama mwaka 1995 kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema.
Filed Under:
NEWS
Saturday 14 May 2016
Post a Comment