Loading...

BREAKING NEWS: BUNGE LA JAMUHURI KWA MARA YA KWANZA LIMEWEZA KUFANYA TUKIO LENYE KULETA HAMASA NA KURUDISHA IMANI KUBWA KWA TANZANIA NI BAADA YA WABUNGE VIJANA BUNGENI KUAMUA KUFANYA MAAMUZI HAYA YA AINA YAKE BILA KUJALI ITIKADI ZAO ZA VYAMA SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA....

WABUNGE vijana wenye umri usiozidi miaka 40 wameanzisha umoja wao, uitwao Umoja wa Wabunge Vijana Tanzania (TYPG) kwa lengo la kuweka msukumo kwa vijana wote nchini, ndani na nje ya Mwenyekiti wa TYPG ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema), alisema uongozi wa Bunge umepokea vizuri mpango huo na kutoa kibali kwa maandishi cha kubariki uwepo wa umoja huo.

Alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah waliahidi kwamba uongozi mzima wa bunge utashirikiana na vijana hao, ili wafikie malengo yaliyokusudiwa.

Alisema TYPG inaundwa na wabunge wote wenye umri usiozidi miaka 40, wakiongozwa na Katiba itakayothibitishwa rasmi Juni 2 mwaka huu, siku umoja huo utakapozinduliwa rasmi.

“Tutaweka kando, tofauti za itikadi za kisiasa katika kuendesha shughuli za umoja huu, ndani na nje ya Bunge ili kuweza kufikia azma ya kuungana kwetu,” alisema.

Akizungumzia uongozi wa TYPG, alisema yeye ni Mwenyekiti na Makamu wake ni Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Katimba (CCM), Katibu Mkuu ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (CCM) Naibu wake ni Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), Mweka Hazina ni mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) na Msaidizi wake ni Hassan Kaunje (CCM), Mbunge wa Lindi Mjini.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top